Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya Yanga Salum Mkemi amejiuzulu wadhifa wake.
Haijafahamika sababu kuu iliyopelekea kiongozi huyo mwenye hadhi ya kuingia kwenye vikao vikuu vya Maamuzi vya klabu ya Yanga kujiweka pembeni.
Katika siku za hivi karibuni, Mkemi amekuwa akituhumiwa na baadhi ya mashabiki wa Yanga kuwa ni miongoni mwa wale wanaopinga mabadiliko katika klabu hiyo.
Hiyo inatajwa kuwa huenda ikawa moja ya sababu iliyomfanya aamue kujiweka pembeni.
Hata hivyo hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na uongozi wa Yanga juu ya ukweli wa kujiuzulu kwake.
Yanga imeitisha Mkutano Mkuu Juni 17, mkutano ambao utaifanyia marekebisho Katiba ya klabu hiyo ili kuruhusu mfumo mpya wa uwekezaji pia kufanya uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa klabu hiyo.