Baada ya Azam FC kutangaza imeingia makubaliano kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Yanga Donald Ngoma, uongozi wa Yanga umesema umeumizwa na kitendo hicho.
“Tulikuwa tunajua Ngoma anaumwa, tumemvumilia kwa muda wa mwaka mzima alikuwa analipwa amekaa ame-relax ana fake leo tunashangaa anakwenda kusaini Azam.”
“Kwa hali ya kawaida hata wewe ukimwambia mwajiri wako unaumwa anakwambia mvunje mkataba ili ukatibiwe zaidi halafu siku hiyohiyo unaajiriwa sehemu nyingine, mwajiri wako atakuelewa vipi?”
“Kitu alichofanya sio cha kibinadamu inaonekana ameweka maslahi mbele kuliko utu, mimi kama mwenyekiti wa kamati ya usajili imeniumiza sana.”