Shirikisho la soka Tanzania TFF leo Jumatano ya May 23 2018 limetangaza majina 30 ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2017/2018.
TFF imetangaza kuwa tuzo za mchezaji bora na nyingine ambazo hutolewa kila mwaka kwa mwaka huu zitatolewa Mlimani City June 23 2018 na TFF wameboresha tuzo hizo zaidi ukilinganisha na mwaka uliopita.
Kwa mwaka 2018 tuzo hizo zimeboreshwa kwa kuondolewa tuzo ya mchezaji bora wa kigeni, lengo likiwa ni kuwajumuisha wachezaji wote kuwania tuzo ya mchezaji bora na kuongezwa kipengele cha tuzo ya muamuzi bora msaidizi.
Hii ndio list ya majina 30 ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora VPL