Msanii wa muziki Bongo, Dully Sykes amesema baadhi ya watu wamekuwa wakihofia kumpa nafasi anayostahili katika muziki kwa madai kuwa huwa hapandi ndege wakati yeye ndiye msanii wa kwanza Bongo kupanda ndege na kwenda kufanya show mkoani Mwanza mwaka 2000.
Muimbaji huyo amesema kwenye muziki wake alitakiwa awe mbali sana kama Wanigeria na kama watu wa Afrika wangesikia muziki wake angewakilisha vizuri Tanzania.
“Lakini watu wanakuwa wananihofia sana, wananiogopa wanajua wakijaribu sijui kitatokea kitu gani,” Dully Sykes ameiambia Choice Fm.
“Wanasema wewe hupandi ndege, mimi napanda kwenye maendeleo nisipande ndege kwa ajili gani?, nafikiri mimi ndio msanii wa kwanza kupanda ndege na kwenda kufanya show Mwanza, kuna wengine walipanda ndege miaka hiyo lakini mimi nilipanda kwenda kufanya kazi,” amesisitiza.
Ameongeza kuwa kipindi hicho wasanii wote walikuwa wanakwenda Mwanza kwa mabasi.