Yondani, Chirwa, Tshishimbi Wapigwa Stop na CAF

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limetoa taarifa kwa klabu za Yanga   na Wolaitta Dicha SC ya Ethiopia ambayo imesema wachezaji wanne wa Yanga na wawili wa Wolaitta hawatacheza katika mechi kati ya timu hizo ambayo itachezwa mwishoni mwa juma hili kutokana na kuonyeshwa kadi mbili za njano katika michezo iliyopita baina ya timu hizo.

Wachezaji wa Yanga watakaohusika ni Kelvin Yondani, Obrey Chirwa, Papy Tshishimbi na Said Juma, ambapo kwa upande wa Wolaitta ni Teklu Tafese na Eshetu Mena.


Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post