Leo April 4,2018 story ambayo imechukua headlines ni kutoka kwa muigizaji mkongwe katika tasnia ya Bongo Movie Riyama Ally hii ni baada ya ku-post maneno ya kashfa kutoka kwa shabiki ambaye alisema kuwa hajui kuigiza zaidi ya kuchamba na kuandika caption ambayo imejibu yale maneno ambayo yalitoka kwa shabiki.
Kupitia instagram account ya Riyama Ally ameandika>>> “Dah kweli ushabiki kitu kibaya sana hasa kushabikia kitu usichokijua nikujibu kwa faida ya wengine, mimi hizo tuzo sizifahamu kabisa na ndio maana sikuwahi ku-post chochote katika ukurasa wangu kwasababu sina taarifa yoyote pia sina taarifa rasmi kutoka kwa wahusika kuwa dada Riyama Ally” -Riyama
“Tulikuchomeka katika tuzo zetu na kingine nilikuta missed calls katika simu yangu nikakuta na ujumbe umeandikwa nikafate kadi siku moja kabla ya tuzo ambayo ni Jumamosi tarehe 31 nikafate kadi kwa wahusika wa tuzo husika tuzo zilikuwa jumapili tarehe 1 skujibu SMS nilikaa kimya na sikutaka kuliongea nilitaka wafanye walichokipanga kisha basi kwani zikifurahi nafsi zao na yangu itafurahi zaidi………..”
Maneno yamekuwa mengi kwenye mitandao ya kijamii baada ya tuzo hizo kufanyika siku ya Jumapili April 1,2018 na kusemekana kuwa tuzo hizo hazikutendewa haki kwa wale waliopokea tuzo hizo kwani kuna waigizaji wengi wenye vipaji.