Prof. Tibaijuka Amwaga Machzozi Hadharani Kisa Hiki Hapa


Mbunge wa jimbo la Muleba Kusini Prof. Anna Tibaijuka amejikuta akimwaga machozi baada ya kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa Diwani viti maalumu na Katibu wa umoja wa wazazi {UWT} wilaya Muleba, Paulina Francis ambaye ametumikia nafasi ya udiwani kwa zaidi ya miaka 27 mpaka mauti yanamkuta.

Akiongea baada ya mazishi Prof. Tibaijuka amesema baada ya kutoka Umoja wa mataifa na kuamua kuingia kwenye siasa, marehemu ndo alikuwa mwalimu wake amemuelekeza vitu vingi hivyo anaamini pengo lake si rahisi kuzibika.

Aidha amesema kuwa kwa awamu hii tayari amewapoteza madiwani watatu katika jimbo lake hali ambayo inampa wasiwasi katika utendaji na utekelezaji wa shughuli za maendeleo, huku akisema kuwa alianza Diwani wa kata Kimwani, akafuata diwani wa kata Buhangaza na sasa Diwani viti maalumu wilayani humo.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post