Mtanange wa Simba na Njombe Mjini Kupigwa Leo
Mtanange wa kiporo cha Ligi Kuu Bara uliokuwa unasubiriwa kwa hamu kati ya Njombe Mji dhidi ya Simba SC unapigwa leo Sabasaba Stadium.
Simba inaingia kucheza mechi hiyo baada ya awali kusogezwa mbele ili kuipa nafasi ya kujiandaa na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry SC.
Kuelekea mechi hii, Simba inaweza ikamkosa mchezaji wake, kiungo Jonas Mkude, aliyeumia kifundo cha mguu japo siku mbili zilizopita alianza mazoezi mepesi chini ya unagalizi wa daktari, Yassin Gembe.
Endapo Simba wataibuka washindi katika mchezo huo, watazidi kuipa kisogo Yanga kwa kufikisha alama 49 dhidi ya 46 za Yanga iliyo nafasi ya pili.
Mara ya mwishi timu hizi zilipokutana, Simba ilishinda kwa jumla ya mabao 4-0 kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi.