Mwanamke mmoja nchini Marekani amefanya shambulio la risasi katika Makao Makuu ya Youtube karibu na eneo la San Francisco na kujeruhi watu watatu na yeye mwenyewe kujiua kwa kujipiga risasi.
Mpaka sasa polisi hawajafahamu nini hasa kilisababishwa mwanamke huyo kufanya shambulio hilo katika ofisi hizo. Mwanamke huyo anakadiriwa kuwa na umri kuanzia miaka 30 na kuendelea.
Inaripotiwa kuwa mwanamke huyo alisogea karibu na mlango wa kutokea wa ofisi hizo na eneo la kulia chakula wakati wa chakula cha mchana na kuanza kufanya shambulio hilo
Tags
Kimataifa