Huu Hapa Ujumbe wa Elizabeth Michael “Lulu” Kutoka Gerezani


Inawezekana ukawa miongoni mwa watu walio-miss kuona au kusikia kazi za muigizaji Elizabeth Michael “Lulu” maana tokea apelekwe jela kutumikia kifungo chake cha miaka miwili imekuwa ngumu kusikia au kuona kazi zake za sanaa.

Hizi ni salamu zake kwa mashabiki kutoka kwa mtu wake wa karibu ambaye ni Dr Cheni ameandika salamu hizo kupitia instagram account yake.

>>>“Hongera sana @elizabethmichaelofficial( LULU)  Kwanza niwapongeze kwa hii program nimekuwa mfuaatiliaji na naamini itakuwa na ‘Impact’ kubwa kwenye jamii. Kikubwa mimi Mahsein @drchenitz ni Muwakilishi, nimeleta ‘pic kadhaa za Pads ambazo zitakuwa msaada kwa Wasichana wakitanzania.”

” Huu ni mzigo wa Elizabeth Michael (LULU),  Ameomba niwasilishe kwenu. Nimekuwa nikimtembelea mara kadhaa kumjulia hali na yeye ameomba ashiriki kwenye kampeni hii ingawaje hayupo. Yupo (jela) Zaidi amesema niwaambie. ANAWAPENDA saana, na anawataka mabint wa kitanzania wawe huru katika kutimiza malengo yao, wasikate tamaa na Mungu atawasimamia.”


Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post