Lolote linaweza kutokea Etihad leo, Liverpool mujiandae kisaikolojia

Baada ya kupokea vipigo viwili mfululizo, hii leo kocha Pep Gurdiola atajaribu kupindua matokeo ya kwanza ya mechi ya Champions League waliyofungwa mabao 3 kwa 0 na Liverpool wiki iliyopita.
Inawezekana kweli Liverpool wakapigwa, yaah inawezekana ukizingatia kwamba mara ya mwisho kwa Liverpool kutembelea Etihad walikula bao 5-0, kipigo hiki kinawapa matumaini City kufanya hivyo tena.
Lakini ushindi huu wa mabao 5-0 wa Manchester City ulikuwa ushindi pekee kwa vijana wa Pep Gurdiola kwa Liverpool katika michezo yao 9 iliyopita katika michuano tofauti, wakipoteza mechi 6 na kusuluhu 2.
Katika michezo yao 13 iliyopita ya City katika uwanja wao wa nyumbani kwenye michuano ya Champions League wamepoteza mchezo mmoja tu, mchezo huo ulikuwa dhidi ya Fc Basel katika raundi ya mwisho.
Manchester United waliifunga City mechi 3 katika msimu wa 2009/2010 na hakuna timu nyingine ilifanya hivyo tena, kama Liverpool watashinda mechi ya leo nao watakuwa wameifunga City mara 3 katika msimu mmoja.
Tayari Liverpool wana mabao 31 katika msimu huu wa Champions League, kama wakifunga tena leo baasi watakuwa wameikuta/kuipita rekodi ya Manchester United ya kufunga mabao 32 msimu mmoja wa CL(2002/2003).
Mara ya mwisho kwa Pep Gurdiola kupoteza michezo miwili mfululizo ya Champions League ilikuwa 2013-2014 katika mchezo wa nusu fainali wakati huo akiwa Bayern Munich wakicheza dhidi ya Real Madrid.
Uwezo wa City unafahamika kabisa na haitakuwa jambo la ajabu kama Man City atamfunga Liverpool japo pia naamini Liverpool watapata bao leo pale Etihad kutokana na namna mabeki wa City wanavyocheza timu yao ikiwa katika presha

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post