Ivo Mapunda Akiri Uwepo wa Ushirikina Kambini


Mhemko wa pambano la Simba na Yanga umepanda, presha ni kubwa kila kona. Shaffih Dauda imekutana na mlinda lango wa zamani wa klabu ya Simba Ivo Mapunda na kufanya naye mahojiano kuhusiana na pambano hilo.
Mapunda ameongea mengi ikiwemo suala la ushirikina, imani za kishirikina zimekuwa zikitawala sana katika soka la Tanzania na Afrika kwa ujumla na Ivo amekiri kuwepo kwa imani hizo katika soka la Tanzania.
Ivo amekiri kwamba wakati akiichezea Simba walikiwa wakifanya ushirikina, japokuwa Ivo yeye amekana kushiriki moja kwa moja katika mambo hayo ila amesema kulikuwa na wataalamu ambao walikuwa wanawafuata uwanjani. 
“Katika vyumba vya kubadilishia nguo walikuwa wanakuja watu wanatupa vitu vya kuvaa ambavyo ni vya kishirikina, mimi sikuwa nafanya hivyo, mara nyingine nilikuwa natupa chooni au naficha kwenye begi.” 
Ivo anasema hakuwa anaamini katika mambo hayo yaliyokuwa yakifanyika Simba (uchawi), kwani kama ni kweli uchawi ungekuwa upo baasi hao waganga wangemsaidoa kwenda kuchukua au kucheza nafasi ya De Gea. 
Kuhusu taulo lake ambalo lilikuwa likizua kizaa zaa mara nyingi likizaniwa kuwa na ushirikina, Mapunda amekanusha kuhusu ushirikina katika taulo hilo na kusema hakuwa anatumia taulo jilo katika uchawi bali alikuwa akiandika maneno ya biblia katika taulo hilo. 
Ivo amekiri kwamba kuelekea katika mchezo huu Simba wanaonekana kuwa na kikosi kizuri zaidi kwani first eleven yao inaonekana kukamilika sana pamoja na wachezaji wa akiba kuliko kikosi cha Yanga.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post