Binti Aliyetumia YouTube Kujizalisha Mwenyewe Hotelini

Kwenye dunia ya sasa, teknolojia imekuja na faida na hasara zake. Kutoka nchini Marekani binti mmoja wa miaka 22 ameeleza jinsi gani teknolojia imeokoa maisha yake pamoja na ya mtoto wake.

Binti huyo ajulikanaye kama Tia Freeman, kutoka Nashville ameeleza kuwa alikuwa hajui jinsi kama ni mjamzito. Alikuwa anasafiri kwenda Ujerumani na Uturuki kwa ajili ya mapumziko.

Anaeleza kuwa hakuwa amegundua mabadiliko yoyote mwilini mwake tofauti na kuongezeka uzito kidogo hivyo hakuhisi kuwa anaweza kuwa mjamzito.

Alipokuwa kwenye ndege kuelekea Ujerumani anasema alikuwa anahisi maumivu makali ya tumbo, safari nzima na hata walipofika Ujerumani na kwenda hoteli bado tumbo liliendelea kumuuma sana.

Tia anaeleza kuwa alihisi labda alikula chakula chenye sumu na kupelekea kuumwa tumbo kiasi hicho, hivyo aliamua kutafuta kwenye mtandao wa google kujua ni nini kinaweza kuwa kinamsumbua.

Kutokana na maelezo aliyoandika ya anavyojisikia, aligundua kupitia google kwamba ulikuwa ni uchungu wa kujifungua, kutokana na hilo hakutaka kupiga simu kuomba msaada hivyo alianza kutafuta kwenye YouTube jinsi ya kujifungua.

Alichemsha maji na kuyaweka kwenye beseni kisha kuyapoza na kuingia kwenye beseni hilo na kuanza kujizalisha mwenyewe hadi akafanikiwa na kuchukua kamba yake ya kiatu na kuitumia kufunga kitovu.

Kwa bahati nzuri, Tian anasema alifanikiwa kujifungua mwenye tena haraka sana na kesho yake alijiandaa na kwenda uwanja wa ndege kupanda ndege ili aende Uturuki.

Wahudumu wa Uwanja wa ndege walishangaa kuona jana yake alipita akiwa na mtoto na kesho yake tu alikuwa na mtoto na wakahisi kuwa pengine alikuwa amemuiba mtoto huyo.

Alipojielezea ilikuwaje akajifungua, Kampuni ya ndege ya Turkish Airline ilimlipia hoteli kwa wiki mbili mjini Istanbul ambapo alikuwa akiangaliwa na maafisa wa matibabu pamoja na mtoto wake.

Mkasa huu wa binti huyu wa miaka 22 kutumia video ya youtube na kuweza kuzaa akiwa peke yake kwenye chumba cha hoteli imesisimua watu wengi na kuzua mijadala kwenye mitandao ya kijamii. 

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post