Baada ya Kukamilisha Matibabu Lissu Kutua Dar Siku Hii

MBUNGE wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu (50) aliyelazwa nchini Ubelgiji anatarajiwa kurejea nyumbani siku yoyote kuanzia juzi, baada ya madaktari kumaliza kumpatia matibabu, amesema.


Lissu ambaye amekuwa hospitalini tangu Septemba 7, mwaka jana aliposhambuliwa kwa risasi nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma, aliliambia Shirika la Utangazaji la BBC juzi, kuwa kwa sasa hana tena kidonda cha risasi na yupo tayari kurudi nyumbani.

“Sina tena kidonda cha risasi, nilipigwa mara 16, sina tena kiungo kilichovunjwa. Nilikuwa nimevunjwa mguu mmoja mara tatu, mikono yote ilikuwa imevunjwa, nilikuwa na risasi nyingi mwilini, na vidonda vingi,” alisema Lissu.

Lissu alisema analazimika kurundi nchini kwa kuwa yeye ni Mbunge, Kiongoziwa Upinzani Bungeni naWaziri kivuli wa Sheria na Katiba. Alisema kwa majukumu hayo hawezi kwenda mafichoni. “Siwezi kwenda mafichoni, siwezi kuikimbia nchi yangu,nitarudi Tanzania,” alisema.

“Mimi ni mbunge, mimi ni kiongozi bungeni, ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, mimi ni msemaji wa sheria na katiba wa chama changu,” aliongeza Lissu.

Hata hivyo, akizungumza na Nipashe jana kaka wa Lissu, wakili Alute Mughwai alisema familia bado haijapokea taarifa ya siku anayotarajia kurudi. Alisema familiainachofahamu ni kuwa Lissu amefanyiwaoperesheni ya 19 wiki chache zilizopita, hivyo kutakuwa na uangalizi wa afya yake.



“Hayo mahojiano aliyofanya juzi sijayaona, nitawasiliana naye leo jioni (jana) nimsikilize, lakini sisi kama familia hatujapata taarifa yoyote lini atarudi, wala hatuwezi kujua haditupewe taarifa na hospitali,” alisema wakili Mughwai.

Lissu alipoulizwa na BBC endapo amepata msaadawa matibabu kutokaserikalini, alisema chombo pekee chenye wajibu wa kumgharamia matibabuyake ni Bunge na “siyo serikali, wala Ikulu, wala mtu yeyote.”

Credit: Nipashe April 30, 2018. 

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post