WASTARA Juma Ataka Mume, Ataja Masharti yake !


Msanii wa filamu nchini Wastara Juma amedai anawachukia wanaume wenye rangi nyeupe kwasababu wanakuwa na matatizo mengi pindi anapokuwa nao katika mahusiano ya kimapenzi ndio maana kwa sasa anawapenda weusi kama aliyokuwa nayo marehemu Sajuki.

Wastara amebainisha hayo wakati alipokuwa anajibu miongoni mwa maswali yaliyokuwa yanaulizwa na mashabiki zake waliokuwa wanataka kufahamu ni mwanaume wa aina gani Wastara anamvutia kuwa naye katika mahusiano ya kimapenzi au kwa sasa endapo atatokea.

"Mimi kiukweli namtaka mwanaume ambae anajiamini ambae hata tukitembea mbele za watu hawezi kuona aibu, anaejali, mwenye mapenzi ya dhati, awe mwanaume wa kweli yaani asiwe 'Punga' ila asiwe na rangi nyeupe maana nawachukia sana wenye rangi hiyo, nampenda mwenye rangi nyeusi", amesema Wastara.

Aidha, Wastara amesema kipindi cha awali alipokuwa anaanza kujihusisha katika masuala ya mapenzi alikuwa na vigezo vingi alivyokuwa anavitaka awe navyo mwanaume kama kifua kikubwa, Six Pack na vinginevyo.

"Kwa sasa sitaki vigezo kwasababu nimejifunza mengi kutoka kwa marehemu Sajuki maana mume wangu alikuwa na Six Packs za ukweli lakini alipokuwa anaumwa zote zikaondoka 'so' kutoka hapo nimejifunza kupenda jinsi mwanaume alivyo maana vingine vinakuja na kuondoka wakati wote", amesisitiza Wastara.

Kwa upande mwingine, Wastara amesema yupo tayari hata sasa kuolewa na mwanaume mwingine ambaye wataridhiana wenyewe kwa kuwa dini yake ya kiislamu inampa fursa ya kuolewa mpaka pale kifo chake kitakapomchukua endapo hatakuwa katika ndoa.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post