Chelsea ndio basi tena UEFA Champions League


Baada ya kumalizika kwa baadhi ya game za UEFA Champions League hatua ya 16 bora msimu wa 2017/2018, game ya mwisho ya marudiano ya hatua ya 16 bora kati ya FC Barcelona dhidi ya Chelsea iliyochezwa katika uwanja wa Camp Nou ilikuwa inasubiriwa zaidi.

Matokeo ya game hiyo yalikuwa yanasubiriwa zaidi kutokana na game hiyo kuzikutanisha timu ambazo zinarekodi nzuri katika michuano hiyo miongoni mwao lakini game ilikuwa 50 kwa 50 yoyote anaweza kuchukua ushindi kutokana na mchezo wa kwanza uliyochezwa London ulimalizika kwa sare ya 1-1.

Chelsea wakiwa ugenini usiku wa leo wamejikuta wakikubali kipigo cha magoli 3-0, hivyo Barcelona wamefuzu kwa jumla ya magoli 4-1, magoli ya FC Barcelona ya leo yalifungwa na Lionel Messi aliyefunga mawili dakika ya 3 baada assist safi ya Suarez na dakika ya 63 na Osmane Dembele dakika ya 20.

Ushindi huo sasa unaifanya FC Barcelona kuungana na timu za JuventusAS RomaSevilla, Real MadridFC Bayern Munich,Liverpool na Man City zilizokuwa tayari zimefuzu robo fainali, hivyo kwa sasa wanasubiri droo ya UEFA kufahamu kila timu itakutana na timu ipi robo fainali.

Ikumbukwe tu kufunga magoli mawili katika mchezo wa leo kwa Lionel Messi kumemfanya kufikisha jumla ya magoli 100 UEFA Champions League lakini likiwa ni goli la 20 kwa kuvifunga vilabu vya England katika michuano hiyo lakini Barcelona wao wamelinda rekodi yao ya kutowahi kuruhusu magoli mawili katika game za mtoano 

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post