Mahakama ya Mwanzo Usambara mkoani Tanga imemhukumu kwenda jela
miezi mitatu Swabaha Shosi ambae alishawahi kushika headlines kwa kulia mbele
ya Rais Magufuli wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria February 2, 2017.
Hakimu wa Mahakama hiyo Khadija Kitogo amemtia hatiani kwa
kuingia eneo lisiloruhusiwa kisheria.
Swahaba alifikishwa Mahakamani hapo August 9, 2017 akikabiliwa
na shtaka la kuingia Chongoleani ambako hakuruhusiwi Raia kuingia.
Mahakama ilielezwa kuwa aliingia katika eneo lililokuwa
limetengwa kwa ajili ya ujio Rais Magufuli na Yoweri Museveni walipokwenda
kuzindua mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda mpaka Hoima.
Swahaba alikana mashtaka hayo na kujitetea kuwa alikanyaga eneo
wakati akiandaa eneo kwa ajili ya kuwauzia chakula waliodhuria uzinduzi huo na
kwamba hakuwa peke yake walikuwa wengi.
Hakimu Kitogo akitoa hukumu hiyo amesema baada ya kusikiliza
ushahidi wa pande zote mahakama imemkuta na hatia ya kuvunja sheria ya Makosa
ya jinai.
“Ninampa adhabu ya
kwenda jela miezi mitatu ili iwe fundisho kwa wengine wanaovunja sheria kwa
kuingia maeneo yasiyoruhusiwa”
Tags
kitaifa