Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro kwa kuwakamata watu waliokuwa wanatumia vibaya jina lake kwa kufanya utapeli mtandaoni na kuwaibia watu fedha.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Dr. Jakaya Kikwete ameandika >>>Natoa pongezi nyingi kwa IGP Simon Sirro na @tanpol kwa kuwakamata watu waliokuwa wanatumia vibaya jina langu, la mke wangu Salma na mwanetu Ridhiwani kuwahadaa na kuwaibia Watanzania ninaowapenda sana. Kubainika kwa mtandao huo na kukamatwa ni hatua nzuri ya kupongezwa.
Jakaya Kikwete
✔
@jmkikwete
Natoa pongezi nyingi kwa IGP Simon Sirro na @tanpol kwa kuwakamata watu waliokuwa wanatumia vibaya jina langu, la mke wangu Salma na mwanetu Ridhiwani kuwahadaa na kuwaibia Watanzania ninaowapenda sana. Kubainika kwa mtandao huo na kukamatwa ni hatua nzuri ya kupongezwa.
5:11 PM - Mar 16, 2018
1,348
353 people are talking about this