Hii ni Surprise Nyingine Kutoka Vodacom Tanzania, Instagram sasa ni Bureeee


Tunajua kuwa Instagram ni moja kati ya mtandao bora sana wa kijamii kwa sasa na
habari kubwa Tanzania leo siku ya Jumamosi ni uzinduzi wa INSTAGRAM YA
BURE kutoka Vodacom Tanzania. Uzinduzi huo umefanywa na Linda Riwa ambaye
ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Bidhaa kwa Wateja.

Katika mpango huu Vodacom Tanzania wanakwambia kuwa unapata Instagram
BURE kila unaponunua kifurushi cha Tshs 1,000 au zaidi usambaze na kuangalia
picha BURE ukiwa kwenye mtandao supa pekee Tanzania. Kifurushi hiki
kitakuwezesha kuangalia picha na ukinunua kifurushi chochote cha Pindua Pindua
utapata picha, video na IG stories bure kabisa.
Uzinduzi huo umepambwa na msanii maarufu Vanessa Mdee na mwanahabari
Millard Ayo.


Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post