Baada ya Sakata la Diamond Kufungiwa Nyimbo WCB Wasema Paul Makonda Ndio Atatoa Tamko Kwa Niaba yao


Baada ya Diamond Platnumz kufungiwa na BASATA uongozi wa WCB kupitia meneja Sallam Sk Amesema RC Paul Makonda ndiye atakaye Toa Tamko kuhusu Hilo :

By Sallam Sk 
Habari za muda huu waungwana. Tumepigiwa simu na vyombo vya habari kila sehemu kuulizwa juu ya nyimbo mbili za Diamond kufungiwa, nimeona tukiwa kama taasisi huwaga tunafanya vitu kwa kutokukurupuka sie kama @wcb_wasafi tulipoona taasisi yetu inakuwa kubwa tukaomba ulezi kwa @paulmakonda ambae ni kiongozi wa serikali mwenye kupenda maendeleo ya vijana, kwahiyo nyimbo zote za WCB kabla ya kutoka lazima mlezi wetu azipitie, kuna nyimbo nyingi ameshazizuia na zinazotoka basi ameridhia yeye binafsi zitoke, kwahiyo sioni sababu ya nyimbo ya Hallelujah na Waka kufungiwa kama inavyosemekana maana sisi hatujapata barua ya kuwa nyimbo hizo zimefungiwa na kwa sababu ipi. Kama kweli zimefungiwa basi mlezi wetu ataweza kuongea mengi zaidi yangu mimi. Nawatakia Weekend njema. .

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post