Walichosema AZAM FC kuhusu Mchezaji wao Himid Mao

Azam FC baada ya Himid Mao kumaliza matibabu Afrika Kusini

Ni siku kadhaa sasa zimepita toka nahodha waAzam FC Himid Mao awe nje ya uwanja kutokana na majeruhi na wote tukasikia kuwaAzam FC wamempeleka Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa matibabu.

Taarifa ikufikie kuwa Himid Mao amesharudi Tanzania na afisa habari wa Azam FC Jafari Iddi Maganga ametoa ripoti  yake kuhusu maendeleo yake baada ya kutoka Afrika Kusini na kurudi Tanzania.

“Himid Mao ambaye alikwenda Afrika Kusini kwa matibabu yeye amesharejea lakini kama tulivyowaambia awali Himid Mao tutaendelea kumkosa uwanjani kwa takribani wiki tatu lakini amerudi na ripoti ya daktari wake ambayo amepatiwa kule Cape Town Afrika Kusini na atakuwa chini ya uangalizi wa daktari wa Azam FC”>>>Jafari Iddi

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post