Guardiola anaweza ingia matatizoni baada ya kudai uhuru wa Catalonia

Kocha wa Club ya Man City ya England Pep Guardiola amejikuta akiingia matatizoni na chama cha mpira cha England FA, baada ya kuonekana akisapoti jimbo la Catalonia la nchini Hispania kudai uhuru wake kuwa kama nchi uhuru.

Pep Guardiola ni miongoni mwa wahispaniola wanaounga mkono jimboa la Cataloniakujitenga na Hispania na kupata uhuru kama nchi lakini baada ya kuonekana Pep Guardiolakatika baadhi ya mechi zake ameonekana akivaa riboni ya kusapoti Catalonia kupata uhuru wake amezua utata.

Baada ya kuonekana hivyo chama cha soka England FA kimetangaza kutaka kumuadhibu Pep Guardiola kwa kuonekana akifanya movement za kisiasa katika soka za kudaiwa kusapoti kudai uhuru wa Catalonia katika game za soka zinazosimamiwa na FA.

Pep ambaye kikosi chake cha Man Citykinajiandaa na game ya fainali ya Carabao Cupdhidi ya Arsenal watakayocheza Jumapili ya February 25 2018, amepewa muda na FA hadi Jumatatu saa 20:00 kutolea ufafanuzi uvaaji wake wa ribon hiyo ambayo ameonekana nayo pia katika press conference ya kuelekea game ya fainali ya Carabao Cup.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post