Tetesi za Soka Ulaya leo Jumamosi 24 February 2018



Image captionGuardiola anakabiliwa na marufuku uwanjani iwapo atavaa kipande cha nguo kuunga mkono wafungwa wa kisiasa katika eneo analotoka la Catalonia katika mechi ya Manchester City dhidi ya Arsenal katika kombe la fainali za Carabao siku ya jumapili. (Times - subscription required)

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola amekubali kandarasi mpya na klabu hiyo yenye thamani ya takriban £20m kwa mwaka hadi 2021,ikiwa ni nyongeza ya £3m ya mkataba wake wa sasa. (Mail)

Guardiola anakabiliwa na marufuku uwanjani iwapo atavaa kipande cha nguo kuunga mkono wafungwa wa kisiasa katika eneo analotoka la Catalonia katika mechi ya Manchester City dhidi ya Arsenal katika kombe la fainali za Carabao siku ya jumapili. (Times - subscription required)

Image captionPepe Guardiola kushoto na Arsene Wenger Kulia

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger haamini kwamba Pep Guardiola ameleta kiwango cha juu cha soka alipokuwa Barcelona na Manchester City.(Guardian)

Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 28, amehusishwa na uhamisho wa klabu nyengine lakini mkufunzi wa klkabu hiyo Zinedine Zidane anasema mchezaji huyo wa Wales atakuwa muhimu sana katika kikosi hicho.(Sun)

Image captionPaul Pogba

Maafisa wa Manchester United wanakasirishwa na tabia ya ajenti wa kiungo wa kati Paul Pogba Mino Raiola, ambaye alimwambai mkufunzi wa klabu hiyo Jose Mourinho, kumchezesha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 raia wa Ufaransa. (Times - subscription required)

Jose Mourinho anasema kuwa wachezaji wa Manchester United wanafaa kumuamini . (Mirror)

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionManchester United imeimarisha hamu yake ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Nice Jean Michael Seri

Manchester United imeimarisha hamu yake ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Nice Jean Michael Seri.

Mchezaji huyo wa miaka 26 kutoka - Ivory Coast anaweza kununuliwa baada ya kulipwa dau la £35m katika kandarasi yake (Mirror)

Wachezaji wa Manchester United hawana shaka na mbinu zilizotumiwa na mkufunzi Jose Mourinho katika mechi ya klabu bingwa Ulaya iliotoka sare dhidi ya Sevilla(Manchester Evening News)

Image captionAnthony Martial

Hatma ya Anthony Martial katika klabu ya Manchester United huenda haijulikani baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 bado hajapata kandarasi mpya katikaklabu ya Old Trafford.

Kandarasi ya mchezaji huyo wa Ufaransa inakamilika mwisho wa msimu huu.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post