Liverpool yapanda hadi nafasi ya pili katika jedwali baada ya ushindi mkubwa



Mohamed Salah alifunga bao la lake la sita mfululizo na kuisadia Liverpool kupanda hadi nafasi ya pili katika jedwali la ligi

Mohamed Salah alifunga bao la lake la sita mfululizo na kuisadia Liverpool kupanda hadi nafasi ya pili katika jedwali la ligi kupitia ushindi mzuri uliowafurahisha mashabiki wake dhidi ya West Ham.

Emre Can aliiweka kifua mbele timu hiyo ya mkufunzi Jurgen Klopp kupitia kona-likiwa ni bao la 100 la Liverpool msimu huu baada ya Salah kugonga mwamba.

Salah hatahivyo alifunga bao la pili kupitia mkwaju wa kimo cha nyoka kufuatia kazi nzuri ya Oxlaide Chamberlain kabla ya mshambuliaji mahiri Roberto Firmino kuongeza bao la tatu baada ya makosa ya kipa Adrian.

Shambulizi la chinichini la Michail Antonio liliwapatia West Ham bao la kufutia machozi lakini Mane ambaye alikuwa amegonga mwamba awali akafunga bao la nne .

Matokeo ya mechi nyengine:

Leicester 1-1Stoke

Bournemouth 2-2 Newcastle

Brighton 4-1 Swansea

Burnley 1-1Southampton

West Brom 1-2 Huddersfield

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post