Club ya Man City inayofundishwa na kocha Pep Guardiola usiku wa February 25 2018 ilifanikiwa kutwaa taji lake la kwanza msimu wa 2017/2018 dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Wembley jijini London, game hiyo ilikuwa ni game ya fainali ya Carabao Cup.
Pep Guardiola amefanikiwa kuiongoza Man City dhidi ya Arsenal kupata ushindi wa magoli 3-0, magoli ambayo yalifungwa na Sergio Aguero dakika ya 18, Vincent Kompany dakika ya 58 na goli la mwisho likafungwa na David Silva dakika ya 65.
Kutwaa taji hilo kwa Man City kunawafanya wafikishe jumla ya mataji matano ya Kombe la Ligi, huku Liverpool ikisalia kama club pekee England iliyowahi kutwaa taji hilo mara nyingi zaidi ya timu zote ikitwaa mara nane, Arsenalwao leo wanakuwa wamepoteza fainali yao ya sita ya Kombe la Ligi kati ya fainali nane walizowahi kucheza.