Manchester United watoka nyuma na kuwashinda Chelsea 2-1
Jesse Lingard alifunga bao lake la 13 msimu huu
Manchester United imerudi katika nafasi ya pili baada ya Jesse Lingard kuwapa ushindi kwenye mechi kali dhidi ya Chelsea huko nyumbani Old Trafford.
Iliwalazimu Manchester United kufanya kazi ya ziada baada ya William kuiweka Chelsea kifua mbele kipindi cha kwanza.
Baada ya mapumziko United walijipanga ambapo Romelu Lukaku alimtangulia Marcos Alonso nakuisawazishia Manchester na kuwa bao lake la kwanza dhidi ya klabu yake ya zamani.
Lukaku kwa mara nyingine tena akampa Lingard mpira msafi zikiwa zimesalia dakika 15 mechi ikamilie na bila kuchelewa akasukuma wavuni.
Chelsea watabaki katika nafasi ya tano baada ya Tottenham kuwashinda Crystal Palace 1-0 mapema leo.
Lukaku alifunga bao lake la kwanza dhidi ya Chelsea
Mada zinazohusiana