#Habari:Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amelipangua baraza lake la mawaziri huku akiunda wizara mpya moja na kuteua Manaibu waziri wawili wapya ikiwa ni hatua ya kuimarisha utendaji wa serikali yake.
Taarifa ya Ikulu iliyosainiwa na Katibu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na ITV kupata nakala inaonesha Dkt. Shein kuunda wizara mpya ya habari,utalii na mambo ya kale ambayo itaongozwa na Mhe. Mahmud Thabit Kombo ambaye alikuwa waziri wa afya,pia ameunda wizara ya vijana,utamaduni,sanaa na michezo ambayo itaongozwa na Balozi Ali Karume aliyekuwa waziri wa ujenzi,mawasiliano na usafirishaji.
Mawaziri wapya waliobadilishwa wizara ni Dkt. Sirra Ubwa Mamboya anakuwa waziri mpya wa ujenzi,usafirishaji na mawasiliano, huku mawaziri waliobadilishwa ni Mhe. Rashid Ali Juma na kuwa waziri wa kilimo,mifugo maliasili na uvuvi huku waziri wawizara hiyo Mhe. Hamad Rashid anakuwa waziri wa afya,manaibu waziri wapya ni Dkt. Makame Ali Ussi naibu waziri wa kilimo,mifugo na uvvui na Mhe. Hassan Khamis Hafidh anakuwa naibu waziri wa biashara na viwanda.