Conte: Tutailaza Barcelona mechi ya marudio



Chelsea iligonga mwamba wa goli mara mbili huku Willian akitekeleza mashambulizi kutoka nje kabla ya raia huyo wa Brazil kufunga katika jaribio lake la tatu

Mkufunzi Antonio Conte amesema kuwa Chelsea "itajaribu kufanya kitu muhimu'' kwa kuibandua Barcelona katika kombe la vilabu bingwa Ulaya baada ya sare 1-1 katika awamu ya kwanza.

Willian aliiweka kifua mbele The Blues lakini Lionel Messi alisawazisha dakika 15 kabla ya mechi kukamilika baada ya makosa ya Andreas Christensen katika mechi ya kufuzu katika robo fainali ya kombe hilo.

Barcelona ambayo iko pointi saba juu ya La Liga haikutekeleza mashambulizi yoyote makali hadi waliposawazisha.

''Tulikuwa tunakaribia kuwafunga'', alisema mkufunzi huyo wa Chgelsea. ''Tulifanya kosa moja , ni aibuna tumevunjwa moyo na matokeo''.

Chelsea iligonga mwamba wa goli mara mbili huku Willian akitekeleza mashambulizi kutoka nje kabla ya raia huyo wa Brazil kufunga katika jaribio lake la tatu kupitia shambulio alilotekeleza akiwa maguu 20.

Hatahivyo dakika 13 baadaye , Christensen alifanya makosa kwa kutoa pasi mbaya iliochukuliwa na Andres Iniesta aliyeshirikiana na Messi ambaye alifunga bao lake la kwanza la vilabu bingwa dhidi ya klabu hiyo ya London.

Christensen mwenye umri wa miaka 21 alikuwa ameichezea Chelsea mara tatu pekee kabla ya msimu huu lakini ameshirikishwa sana msimu huu huku beki wa kati Gary Cahil akipumzishwa.


Christensen mwenye umri wa miaka 21 alikuwa ameichezea Chelsea mara tatu pekee kabla ya msimu huu

Hatahivyo Conte alimtetea beki huyo wa Denmark licha ya makosa yake yalioipatia Barca bao muhimu ugenini huku awamu ya pili ya mechi ya marudiano ikichezwa tarehe 14 mwezi Machi nchini Uhispania.

''Tulicheza vizuri sana'' , alisema raia huyo wa Itali. ''Tunazungumzia kuhusu mchezaji mdogo sana. Ni vyema kwamba anaweza kucheza katika mechi kama hii akionekana mchezaji aliyekomaa. Alikuwa miongoni mwa wachezaji wazuri sana usiku huu. Ni vigumu kumtaja mchezaji mmoja lakini nadhani Christensen alicheza mechi kubwa na nilifurahishwa na mchezo wake. Tulifanya kosa moja lakini tunajua ukicheza na wapinzani kama Messi, Iniesta na Suarez unapofanya makosa unagharamika''.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post