Zijue Faida za Kiafya za Kunywa Maji ya Moto




Kuna tiba nyingi za kitabibu zilizogawanyika katika makundi mbalimbali. Kuna zile za hospitali ambazo ni lazima zinunuliwe, lakini kuna tiba ambazo kwa ushauri wa daktari hata wewe unaweza kuziandaa bila kutumia gharama kubwa. Moja ya tiba hizo ni kunywa maji ya moto.

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, maji moto yanatibu magonjwa mengi ikiwemo figo, kutoa sumu mwilini na kuyeyusha mafuta tumboni. Pia hurahisisha mzunguko wa damu, huondoa sumu kwenye ubongo na kusafisha haja ndogo.

Kunywa maji ya moto kila unapotaka kwenda kufanya kazi ya nguvu au mazoezi iwe kama kinga na inashauriwa kila siku unywe glasi nane ili kutoa taka na kila kisichotakiwa kubaki mwilini, kupitia jasho. Wataalamu wa afya wanasema kuwa ni vyema pia kunywa maji ya moto yenye ndimu au limao kabla ya kifungua kinywa ili kurahisisha mfumo wa mwili kwa siku nzima.

Mwinyimvua Pazi, Mtaalamu wa Chakula na Lishe kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anasema kuwa maji yanarahisisha uyeyushaji wa chakula na mafuta mwilini, hivyo kutokana na umuhimu huo ni vyema kunywa maji ya moto yatakayofanya kazi haraka na kwa ufanisi mkubwa bila kuchosha figo.

Anaitaja faida nyingine ya kunywa maji ya moto kuwa ni kutoa sumu zilizopo kwenye mishipa ya fahamu na kuisaidia figo kufanya kazi kikamilifu, Fahamu aina za maumivu ya kichwa kwenda kufanya mazoezi, kitu kinachoweza kuzidisha maumivu au maji kucheza wakati wa kukimbia kama mazoezi ya kukimbia.

Lakini yakiwa ya moto ni kama umekunywa chai au kula chakula cha kawaida, tofauti na maji baridi ambayo yanagandisha na kuilazimisha figo kuyeyusha kwanza na kisha kuchuja. Anashauri umuhimu wa kunywa maji moto kabla ya kufanya mazoezi kuwa ni kujiandaa kwa ajili ya kuchuja jasho ambalo litatoa sumu.

Maji yakiwa ya moto yakifika kwenye figo yanaanza kufanya kazi moja kwa moja, kuliko yakiwa ya baridi yanaweza kusumbua kwa kuwa ni lazima yapate joto la mwili kwanza kabla ya kuanza kufanya kazi.

“Ukiachilia kusubiri yachemke, pia ni kumuepusha mtumiaji na hatari ya kuumwa tumbo kutokana na kunywa maji ya baridi bila kuweka kitu tumboni na  Maji Ya Moto Yalivyo Na Faida Mwilini anasema Mwinyimvua. Mwinyimvua anaongeza kuwa maji ya moto ni mazuri hata kwa kupata choo, kwa vile yanarahisisha uyeyushaji na uchambuaji wa kinachotakiwa na kisichotakiwa.

Wanaokunywa ya baridi wana uwezekanao mkubwa wa kupata haja kubwa kwa shida. Vilevile, Mwinyimvua anashauri kuwa ni vyema kunywa maji moto yaliyochemshwa na kuyaacha yapoe na kuwa ya uvuguvugu na kuongeza limao na asali ambapo mbali na kuongeza ladha, asali na limao vina faida kiafya.

Gayl Canfield, Mkurugenzi wa Lishe kutoka katika Kituo cha Biashara cha Pritikin Longevity kwenye Mji wa Miami, Florida nchini Marekani, anasema kuwa kunywa maji ya uvuguvugu au ya moto ni vyema kwa kuwa hufanya kazi moja kwa moja kutokana na hali ya tumbo kuwa na joto muda wote. Canfield anasisitiza, “Maji ni muhimu kwa mwili wako, yakiwa ya moto ni bora zaidi, kwa kuwa yanatoa rangi ya njano ya mkojo na kuufanya uwe msafi na wenye rangi angavu.”

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post