Wanachi jimbo la Zitto Kabwe waililia serikali

Mji wa Kigoma ujiji hauna huduma ya maji kwa siku tano sasa baada ya mamlaka ya maji safi na taka kukatiwa umeme na kushindwa kutoa huduma.

Hali ambayo imesababisha wananchi kuhangaika usiku na mchana kutafuta maji maji ya chemchem na visima, na kuiomba serikali kuhakikisha tatizo hilo linakwisha mapema ili kuepuka maradhi wanayoweza kuyapata, kutokana na ukosefu wa huduma ya maji ambayo sasa wanalazimika kutumia maji yasiyo salama.

Akizungumzia hali hiyo kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na taka Kigoma Ujiji  Mhandisi Mike Jones, amesema sababu ya kukatiwa umeme ni kutolipa kwa wakati ankara za umeme lakini suala hilo linashughulikiwa haraka ili kuweza kutatua suala hilo

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post