Kamanda Mambosasa akemea Trafiki waonevu

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa atoa maelezo ya wa jinsi Askari wa Usalama Barabarani(Trafiki), wanavyotakiwa kutekeleza majukumu yao.

Kamanda Mambosasa ameeleza kuwa Trafiki wamekuwa na tabia ya kusimamisha gari, kuomba leseni na kukagua kama dereva au mmliki wa gari ana vitu kama stika ya bima, taa, magurudumu, mtungi wa gesi ya kuzimia moto na viakisi mwanga(Reflector).

Akafafanua kuwa Askari akisimamisha gari ni lazima akueleza sababu za kukusimamisha. Pia ni lazima aeleze anataka kukagua nini katika gari lako

Akaongeza kuwa Trafiki wanatakiwa kutumia busara kumtoza faini Dereva ambaye gari lake lina matatizo ya taa kwa kuwa huenda hatumii gari hilo nyakati za usiku.

Ufafanuzi huu umekuja wakati ambapo watumiaji wa vyombo vya moto wamekuwa wakilalamikia vitendo wanavyoviita vya kionezi kutoka kwa Askari wa Usalama Barabarani pamoja na kutozwa faini kubwa kwa makosa madogo

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post