Serikali kupitia Wizara ya Madini,imetoa siku 14 kwa uongozi wa kiwanda cha Saruji cha Dangote Mkoa wa Mtwara kuingia mkataba na wachimbaji wadogo wa gypsum.
Mhe. Biteko
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Madini, Doto Biteko ambapo ametoa agizo hilo baada ya kutembelea kiwanda hicho na kuzungumza na uongozi wa kiwanda hicho.
Mhe. Biteko amesema mikataba hiyo inapaswa kuwa na kipengele cha kuwalipa ndani ya siku 30 baada ya kiwanda kukusanya gypsum kutoka kwa wachimbaji hao, lengo likiwa ni kuleta ufanisi na tija katika biashara zao.
Kwa upande mwingine, Biteko amesema wachimbaji hao wamekuwa wakilalamikia kucheleweshewa malipo yao baada ya kupeleka kiwandani bidhaa zao hivyo ameagiza jambo hilo limalizike na watu wapate haki zao.
Tags
kitaifa