Leo January 21, 2018 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imetoa tahadhari kwa umma kuhusu ugonjwa wa homa ya CHIKUNGUNYA ambao umeripotiwa na vyombo vya habari kutokea nchini Mombasa nchini Kenya lakini bado Shirika la Afya Duniani (WHO) halijatoa taarifa rasmi.
Wizara ya Afya imetoa tahadhari ya ugonjwa wa CHIKUNGUNYA kutokana na muingiliano mkubwa uliopo kati ya nchi ya Kenya na Tanzania.
Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na homa kali na maumivu ya viungo, misuli, kichefuchefu na uchovu.
Ripoti za awali kabisa za kuwepo ugonjwa huo wa CHIKUNGUNYA zilipatikana katikati ya mwezi uliopita ambapo kilichofuatia kilikuwa ni kukusanya sampuli za damu na kuziwasilisha kwenye maabara kwa ajili ya uchunguzi.
Ugonjwa wa CHIKUNGUNYA unaweza kupunguzwa kwa kuchukua hatua kadhaa ikiwemo kuhakikisha mazingira ni masafi ili kuepusha mazalia ya mbu.