Sanchez aliazima hadi viatu vya Mpira mpaka kufikia hapo alipo

Tayari Alexis Sanchez amesaini mkataba wa kuitumikia Manchester United ambapo sasa nyota huyo wa Chile atakuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika klabu ya Manchester United(£600,000 kwa wiki).

Lakini ndoto ya Alexis kwenda United haijaanza leo, mmoja kati ya wachezaji wenzake wa Chile alisema tangu Alexis akiwa mtoto alijituma sana akiamini kwamba siku moja atakuja kuichezea Manchester United.

Katika interview yake ya kwanza na Manchester United Alexis amekiri kwamba hapo mwanzo ameshawahi kuwasiliana na Alex Ferguson kuhusu kujiunga na Manchester United na SAF alimfanya atamani zaidi kujiunga na United.

Lakini wapi Sanchez ametokea? Kama ilivyo kwa wacheza soka wengi kutoka bara la America Kusini kutokea kwenye maisha magumu baasi ndivyo hivyo pia kwa Alexis Sanchez alitokea maisha hayo hayo.

Familia ya wakina Sanchez haikuwa na pesa na kila mtu kwenye familia yao alipaswa kupambana ili familia yao na mama yao aitwaye Martina waweze kupata mkate wao wa kila siku.

Sanchez alikuwa akimpenda sana mama yake na tangu akiwa mtoto alihakikisha mama yake anafurahi na hii ilimfanya kufanya kazi mbali mbali ikiwemo kuosha magari ili apate pesa ya kumpelekea mama yake chakula.

Baadaye Sanchez alianza kucheza mpira mtaani na marafiki zake wanasema walikuwa wakicheza soka kwenye lami ambapo ilikuwa inawaunguza na hii ikamfanya Alexis awe anaazima viatu kwa watu ili akacheze soka.

Shida kubwa katika ukuaji wa Alexis ilikuwa ni mji aliototokea, Tocopilla ulikuwa mji ambao ulijawa na bishara kubwa za madawa na mambo ya matumizi ya bunduki na hii ilitishia ndoto ya Alexis kuwa mwanasoka mkubwa.

Baadae kocha wa utotoni wa Alexis Sanchez aliamua kumtoa nje ya Tocopilla na kuanza kumtaftia timu na ndipo baadae nafasi ya Sanchez kwenda Serie A kujiunga na Udinesse ilianza.

Safari ya Sanchez kwenda Udinesse ilikuwa ngumu sana kwa familia yake, na dada yake aitwaye Barbara Argosta anakiri kwamba ni kati ya matukio ambayo yalimuumiza sana kwa kuwa Alexis aliondoka akiea na miaka 16 tu.

Kiwango alichoomesha Sanchez akiwa na Udinesse kiliwashawishi Barcelona kumpigia simu na baadae akajiunga nao akishinda makombe matano kabla ya kutua Arsenal mwaka 2014.

Wakati akiwa Arsenal marafiki zake wengi walioko Chile walishangazwa na Sanchez kwenda Arsenal kwani wengi walifahamu kwamba Sanchez ndoto zake ni Manchester United tu.

Sasa Sanchez ametua United huku akipewa jezi namba 7 na mashabiki wa Manchester United wanasubiri kwa hamu kuona kama Sanchez anaweza kuitendea haki namba hiyo ambayo wengi iliwashinda

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post