Rais wa TFF apata shavu CHAN

Na Mpemba

Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) limemtangaza Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Wallace Karia kuwa Kamishna wa mechi ya fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN.

Karia atasimamia mchezo huo wa fainali utakaowakutanisha wenyeji Morocco dhidi ya Namibia siku ya Jumamosi Januari 27, 2018.

Kabla ya fainali Karia pia alisimamia mechi ya ufunguzi iliyowakutanisha wenyeji Morocco na Mauritania Januari 13, 2018 na mchezo wa pili uliozikutanisha Namibia na Zambia Januari 22, 2018.

Michuano ya CHAN ilianza Januari 13 nchini Morocco ambapo awali ilipangwa kufanyika nchini Kenya, kabla ya CAF kubadili kutokana na nchi hiyo kuchelewa kukamilisha miundombinu kwaajili ya michuano hiyo.

Kwa upande wa Afrika Mashariki nchi pekee iliyokuwa inashiriki ni Uganda ambayo haikufanya vizuri baada ya kuondolewa katika hatua za awali. Tanzania ilitolewa mapema na Rwanda kwenye harakati za kuwania kufuzu.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post