Polisi yatumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji DRC


Waandamanaji walimiminika DRC mnamo 2016 kumshinikiza rais Kabila aondoke madarakani

Polisi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wanaomtaka rais Joseph Kabila aondoke madarakani.

Watu kadhaa wamejeruhiwa na wengine wamekamatwa, wakiwemo waandishi habari.

Maafisa wamepiga marufuku maandamano hayo na huduma za intaneti zimefungwa.

Kanisa katoliki limewataka raia washirika katika maandamano ya amani baada ya misa ya Jumapili - wakibeba bibilia rosari na misalaba.


Kabila aliingia madarakani mwaka 2001 baada ya babake Laurent Kabila kuuawa

Maafisa wa usalama walikabiliana na maandamano hayo kwa kutumia nguvu katika miji tofuati nchini.

Katika mji mkuu Kinshasa, walinda amani wa Umoja wa mataifa wanaarifiwa kutawanywa kujaribu kuwatenganisha waandamanji na vikosi vya usalama nchini.

Kumeshuhudiwa maandamano mengi dhidi ya rais Kabila tangu muhula wake umalizike zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Congo inakabiliwa pia na mizozo kadhaa ya makundi ya kujihami, husuan katika maeneo ya mashariki na kati mwa nchi hiyo.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post