Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli January 28, 2018 ametia saini kitabu cha maombolezo na kutoa heshima za mwisho kwa mwili Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Robert Kisanga nyumbani kwake Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pia wametoa mkono wa pole kwa mke wa Marehemu Mama Maria Kisanga na kufanya maombi ya pamoja na familia ya marehemu.
Jaji Mstaafu Robert Kisanga alifariki dunia January 23, 2018 katika hospitali ya Regency Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Tags
kitaifa