London: Mshukiwa aliyewagonga vijana 3 atorotoka eneo la ajali'

Waathiriwa watatu wa ajali wametajwa ( ukianzia kushoto) ni George Wilkinson, Harry Louis Rice na Josh Kennedy

Mwanamume anayeshukiwa kutoroka kutoka eneo la tukio la ajali ya gari ya kutisha iliyowauwa vijana watatu wa kiume anasakwa na polisi.

Wahanga hao watatu wa ajali waliokufa baada ya gari la Audi kupandaukingo wa barabara mjini London, wametambuliwa kama Harry Louis Rice, George Wilkinson na Josh Kennedy.

Bibi yake George alizulu eneo la ajali katika mji wa Hayes, magharibi mwa London, akasema kuwa familia "imeumia".

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka , 28, ambaye alikuwa ndani ya gari lilipopata ajali , ameshikiliwa kwa tuhuma za kusababisha vifo na uendeshaji gari hatari .

Polisi imesema kuwa inaaamini walau mwanamume mmoja alikimbia baada ya ajali hiyo kutokea katika bara bara ya Shepiston Lane, ijumaa.

Kijana mwenye umri wa miaka 28 alikamatwa na umma kabla kuwasili kwa polisi, kwa mujibu wa walioshuhudia kisa hicho.

Wachunguzi hata hivyo hawajabaini iwapo kuna uwezekano wa kuwemo kwa wasafiri zaidi katika gari hilo jeusi aina ya Audi ,ambalo linaaminiwa kuwa lilikuwa likisafiri kwa kasi kubwa kabla ya kugonga ukingo wa bara bara kutoka kwenye kituo cha mafuta ya petroli cha Esso..

Gari jeusi aina ya Audi clinaaminiwa kupanda ukingo kabla ya kugonga mti wa taa ya barabarani

Waliokufa wawili walikuwa na miaka 16 na mmoja miaka 17, na walikuwa njiani kusherehekea siku ya kuzaliwa kwenye uwanja uliopo karibu wa soka.

Babu yake George Wilkinson , Nigel Goodhand, alikwenda kwenye eneo la tukio Jumamosi .

"Nimevunjika moyo sana. Inaumiza.

"lengo langu halikuwa kukomea hapa, lakini nimelazimika hatimae", alisema.

"Nimekasirika, lakini nimeridhika nimekuona. Tutamkosa sana ."

Taarifa ya polisi mjini London imesema kuwa: "Uchunguzi unaendelea kubaini kikamilifu mazingira ya ajali na idadi ya watu wahusika''

Umati ulikusanyika kwenye barabara ya shepiston kutoa heshma zao kwa vijana waliokufa

Mshukiwa aliyekamatwa anahojiwa katika kituo cha polisi cha kaskazini mwa London.

aliokufa wawili walikuwa na miaka 16 na mmoja miaka 17, na walikuwa njiani kusherehekea siku ya kuzaliwa kwenye uwanja uliopo karibu wa soka

Ndugu na marafiki wakitoa heshma zao kwa vijana watatu waliouawa kwa kufunga baluni karibu na eneo la ajali

Ndugu mmja wa vijana waliouawa kwenye ajali hiyo amefahamishwa na uchunguzi wa mwili utafanyika baadae .

Vijana wengine wawili waliokuwa wamesimama pamoja nao hawakujeruhiwa.

."

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post