Paka wa ofisini: Paka walioajiriwa kazi za ofisini



Paka aliyeajiriwa ofisi ya posta London

Kwa kawaida maisha ya paka ni ya kulala, kula na mara chache kuruka ,baada ya kusinzia kwa muda mrefu.

Lakini baadhi ya paka hufanya kazi kwa ajili ya kukidhi maisha yao na kutekeleza majukumu yao ya kikazi ipasavyo - na wakati mwingine huvalia sare kamili ya kazi .

Hawa ni baadhi ya paka wa Uingereza ambao hufanya kazi zaidi ya kula, kulala na kuzurura.

Paka wa ofisi ya posta

Kwa mujibu wa makavazi ya posta, paka maarufu alikuwa alikuwa ni TibsPaka anayedaiwa kuwa mrefu zaidi duniani

Mnamo mwaka 1868 paka wawili waliajiriwa rasmi kamawawindaji wa panya katika ofisi ya huduma ya kuagiza na kutuma pesa mjini London.

Walilipwa mshahara wa shilingi moja kwa wiki, pesa ambazo zilikwenda kwa wamiliki wao - na walipewa miezi sita ya kipindi cha kuchunguzwa ikiwa kweli wanaimudu kazi hiyo.

Bila shaka walitekeleza majukumu yao ipasavyo kwani mwaka 1873 walitunukiwa kwa nyongeza ya mshahara.

Matumizi rasmi ya paka kwa kazi za ofisini yalienea katika ofisi nyingine.

Kwa mujibu wa makavazi ya posta, paka maarufu alikuwa alikuwa ni Tibs.

wakati Paka Tibs alipokufa mwaka 1964 kulikuwa na wosia wake uliochapishwa katika jarida la Ofisi ya Posta

Alizaliwa Novemba 1950, akiwa na uzito wa kilo 10.4 na kuishi katika kwenye klabu ya vinywaji ya makao makuu ya posta iliyopo kati kati mwa jiji la London.

Paka wa mwisho wa makao makuu ya Posta London alikuwa ni , Blackie,aliyekufa Juni 1984, na tangu wakati huo hakuna paka aliyewahi kuajiliwa pale

Mamlaka za Ubelgiji haziwezi kusahaulika kwani miaka ya 1870s ziliwaajiri paka 37 kuwasilisha mizigo kwa njia ya mifuko isiyowea kuingiliwa na maji ambayo ilifungwa kwenye kola za mashati yao.

Lilikuwa ni wazo lililotolewa na jamii ya wabelgiji kwa lengo la kuwatumia paka wa nyumbani , ambapo walidhani paka hawapewi mwongozo ipasavyo

Wakati wa majaribio ya kazi hiyo, paka walichukuliwa kutoka kwenye vijiji vyao karibu na Liège, na kupelekwa maili chache mbali na kuvalishwa begi lenye bahasha kwa wazo kwamba paka hao wangerejea nyumbani na begi hizo.

Ingawa paka wote na bahasha za ujumbe walizopewa hatimae vilirejeshwa nyumbani , ilibainika kwamba paka wasingefaa kufanya huduma ya bora ya posta kwa hiyo wazo hilo likapuuziliwa mbali.

Paka wa polisi

Kazi ya paka polisi Oscar ni kuwaliwaza kiakili maafisa wa polisi wanapokuwa wamechoka na wakati mwingine kuwa na mfadhaiko wa kiakili

kwa muda mrefu mbwa wamekuwa ni sehemu ya kikosi cha polisi, lakini ni nadra kwa paka kushirikishwa kwa shughuli za kikosi hicho . Lakini katika majira ya joto mwaka 2016, kituo cha polisi cha Durham Constabulary kiliwaajiri wanyama hawa.

Mtoto mmoja wa miaka mitano Eliza Adamson-Hopper aliiandikia polisi akipenekeza kuwa paka waongezwe kwenye kikosi cha polisi

Uteuzi huo uliandikwa kwenye barua iliyochapishwa na mtoto wa miaka mitano Eliza Adamson-Hopper, ambaye alipendekeza paka waongezwe kwenye kikosi hicho.

"paka polisi anaweza kuwa mzuri kwasababu wana maskio mazuri na anaweza kusikiliza hatari. Paka ni wazuri katika kutafuta njia zao kuelekea nyumbani na wanaweza kuwaonyesha polisi njia ," alisema.

Mittens si paka polisi peke yake. Oscar anaishi kwenye kituo cha polisi cha Holmfirth eneo la Huddersfield, ambako kazi yake inahusiana na "kuwaliwaza kiakili maafisa wa polisi ", na paka Smokey ni afisa wa kujitolea katika kituo cha polisi cha Skegness.

Kulingana na msemaji wa polisi wa kituo hicho , "kuwa afisa wa polisi ni kazi inayokupeleka mbio na ya kutia mfadhaiko , kwa hiyo unapotaka kupumzika kama kupunga hewa kidogo , wengi wetu hitoka nje na kukaa kwa dakika chache na Smokey".

Paka mwanajeshi


Katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia jeshi la Uingereza na lile la wanamaji waliwapeleka karibu paka milioni moja kumaliza wadudu wa majini na ardhini

katika zama za kale yapata miaka 9,500 iliyopita paka walikuwa wakitumiwa katika meli za kivita na katika maeneo yenye panya wengi.

Katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia jeshi la Uingereza na lile la wanamaji waliwapeleka karibu paka milioni moja kumaliza wadudu wa majini na ardhini.

Wakati wa Vita ya Pili ya Dunia karibu kila chombo cha majini kilikuwa na walau paka mmoja.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post