George Weah kuapishwa leo kuwa rais wa Liberia



George Opong Weah

Raia wa Liberia wanasubiria kwa hamu tukio hilo la kuapishwa kwa Rais wao George Opong Weah,ambapo wamekesha katika uwanja wa mpira wa taifa,mahala ambapo leo historia ya mwanasoka huyo inajiandika upya kutoka kung'ara katika soka na hatimaye kuingia katika uga wa siasa kuwa rais wa taifa hilo lenye historia ya milima na mabonde kisiasa.

George Weah, maisha yake ya utoto,yalikuwa katika mazingira duni katika mji mkuuwa Liberia Liberia Monrovia, alipata mafanikio makubwa katika medali ya soka na kufanikiwa kuchezea timu kadhaa barani Ulaya ikiwemo Chelsea na AC milan.

Ni Muafrika pekee kuwahi kushinda tuzo mchezaji bora wa FIFA na tuzo ya Ballon.

Weah aliingia katika siasa baada ya kustaafu soka mwaka 2002 na akawa miongoni mwa maseneter katika bunge la Liberia.

Aligombea urais mwaka 2005 ,na Alimshinda Bi Johnson Sirleaf wakati wa duru ya kwanza katika uchaguzi huo lakini kashindwa katika duru ya pili ambapo kambi yake ilisusia kushiriki katika duru ya pili.


Aliyewahi kuwa meneja wa George Weah katika klabu ya Monaco inayocheza ligi kuu ya Ufaransa Arsernal Wenga amealikwa na atakuwepo katika uapisho huo.

Meneja huyo wa Arsenal alikuwa meneja wa Weah katika klabu ya Monaco inayocheza Ligi Kuu ya Ufaransa miaka ya 1990 na amesema hakuwahi kufikiria kwamba wakati mmoja mchezaji huyo angekuwa rais.

Huyu ndiye George Opong Weah ambaye leo anaapishwa kuiongoza Liberia.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post