Kwanini Mapenzi hupungua baada ya Ndoa???

WANAWAKE WOTE WANGEKUWA HIVI HATA BAADA YA NDOA WANAUME WANGETULIA NA KUWAPENDA DAIMA:

 Unakuta wanawake wanakuwa romantic sana kabla hawajaolewa kiasi cha kuwa na mvuto wa kimapenzi kwa wachumba wao hata kuwafanya wawapende na kuona fahari kuongozana nao.

Tatizo ni pale wanapoingia katika ndoa na kujisahau kabisa pasipo kuboresha mvuto wao. Kuwa na mvuto kwa mumeo,mfanye atamani kuwahi kurudi nyumbani wakati wote anapomaliza kazi.

Mfanye atamani kuwa ama kutoka out na wewe,kula chakula ulichopika wewe na kuoga maji uliyoandaa wewe hata kama kazini kwake huduma hizo zinapatikana.

Muda wote atambue hakukosea kuchagua msaidizi wa kuambatana naye.Usibweke kwa mumeo hata kumfanya atamani kuchepuka na mabinti wengine walio romantic. 

Be romantic and sex kwa namna unavyovaa,unavyotembea,unavyoongea naye na hata unavyokaa kama mtoto wa kike. 

Lakini usiigize bali ishi hivyo kama mke unayejielewa na kujiamini.Deka ubembelezwe siyo kukomaa kama ubao ama kisiki cha mpingo.

Mpe mumeo pumziko na furaha kwa manjonjo.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post