Hatimaye Ndoto Imetimia..Jack Wolper Kufunga Ndoa


BAADA ya kupitia misukosuko mingi katika mahusiano ya kimapenzi, malkia wa fashion na mkali wa filamu za Bongo, Jacqueline Wolper huenda akafunga ndoa hivi karibuni mara baada ya kuanika mipango yake ya kwenda kumtambulisha mpenzi wake kwa wazazi.

Japo hajataja jina, Wolper ameeleza kuwa mpenzi wake huyo ameridhia suala hilo kwani naye pia alikuwa akilihitaji toka mwanzo huku akibainisha kuwa amejifunza kunyamaza bila kuweka hadharani mahusiano yake na siku ya leo ndipo anatarajia kumtambulisha nyumbani kwao, Moshi na taratibu nyingine kama mahari kufuata.

ALICHOKIANDIKA WOLPER

Wewe ni mwanaume ambae umejitoa ili tu niwe wako, umetaka tufike mbali kwanza kabla ya mambo mengine (uwende kwa wazazi, (NDOA) pamoja na kwamba mahusiano yangu ya nyuma yalikuwa yana misukosuko mingi ila umemthamini Jacq. Nilipotoka niliteswa sana na mapenzi yaani usaliti, dharau, kukosa na mapenz ya dhati.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post