![Wanamgambo waliulenga msikiti mmoja karibu na eneo la al-Arish](https://ichef.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/DC31/production/_98896365_799b9524-fb44-4895-a4a4-78ce59e5e4d5.jpg)
Wanamgambo wametekeleza shambulio la
bomu na ufyatuaji wa risasi katika msikiti mmoja uliopo kaskazini mwa
eneo la Sinai na kuwaua takriban watu 235 kulingana na chombo cha
habari cha taifa.
Walioshuhudia wanasema kuwa msikiti wa al-Rawda
katika mji wa Bir al-Abeid , karibu na al-Arish ulilengwa wakati wa
ibada ya Ijumaa.
Misri imekuwa ikikabiliana na wanamgambo katika eneo hilo tangu 2013.
Kumekuwa
na mshambulio ya mara kwa mara yanayolaumiwa kutekelezwa na wanamgambo
katika rasi ya Sinai lakini hilo ni shambulio baya zaidi kuwahi
kufanyika.
Picha katika eneo la mkasa huo zinaonyesha damu iliomwagika ndani ya msikiti.
![Ramani ya eneo la al-Arish](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/12A51/production/_98896367_b4af4bb2-3b73-4c5f-b284-ea278a3009aa.jpg)
Ripoti moja inasema kuwa waliolengwa ni wafuasi wa maafisa wa usalama waliokuwa wakitekeleza ibada katika msikiti huo.
Wakaazi wa eneo hilo wanasema kuwa wafuasi wa madhehebu ya Sufi hukongamana katika msikiti huo.
Makundi ya wanajihad likiwemo lile la Islamic State wanawaona wasufi kama watu wasioamini.
Rais Abdul Fattah al-Sisi anatarajiwa kukutana na maafisa wa usalama kuzungumzia kisa hicho .
Tags
Kimataifa