Tunda Afunguka Juu ya Mwanaume Aliyempa Mimba

 Tunda Afunguka Juu ya Mwanaume Aliyempa Mimba



BAADA ya habari kuzagaa kwamba mrembo anayeuza nyago kwenye video mbalimbali Bongo, Tunda Sebastian kuwa na ujauzito wa staa wa Bongo Fleva, ameibuka na kufungukia ishu hiyo.
Akizungumza na Star Mix, Tunda alisema hana ujauzito wa msanii huyo kama watu wasemavyo na kwamba huwa
anamuweka katika mitandao ya kijamii husan Instagram kwa sababu ya kumsapoti katika kazi zake.

“Ndiyo kwanza nasikia kwenu, siyo kweli na sina mimba yake. Huwa namuweka Insta kumsapoti kikazi tu maana ni rafiki yangu sana lakini watu walivyoona hivyo wakaanza kuzusha maneno hayo kwamba ninatoka naye na nina mimba yake. “Kuhusu kunenepa, nimenenepa kwa sababu nimeridhika na maisha mazuri niliyo nayo,” alisema Tunda.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post