Taifa Stars Kufundishwa na Kocha wa UEFA

Taifa Stars Kufundishwa na Kocha wa UEFA




Shirikisho la soka nchini TFF limemtangaza mchezaji wa zamani wa Tanzania Ammy Ninje kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania bara maarufu kama Kilimanjaro Stars.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam afisa habari wa shirikisho hilo Alfred Lucas amesema kocha huyo mwenye leseni A ya ukocha kutoka shirikisho la soka barani Ulaya UEFA ataiongoza Kilimnjaro Stars kwenye michuano ya CECAFA Challenge mwaka huu.
Katika hatua nyingine Alfred amesema kocha Ammy kesho anatarajia kutangaza wachezaji wa kikosi hicho watakaokwenda nchini Kenya kuiwakilisha Tanzania bara kwenye michuano hiyo.
Ammy Conrad Ninje ni mchezaji wa zamani wa Tanzania ambaye amecheza soka na kujifunza ukocha katika nchi za Ulaya na Amerika. Hatua kubwa ambayo amewahi kufikia ni kuwa kwenye benchi la ukocha la timu ya Hull City ya nchini England.
Michuano ya CECAFA Senior Challenge inatarajiwa kuanza Desemba 3 hadi 17 mwaka huu. Kilimanjaro Stars imepangwa kundi A na nchi za Kenya, Libya, Rwanda na Zanzibar.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post