Nyalandu Kufikishwa Kwenye Mikono ya Sheria



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjZgt28t-m2JDbbsUd0cSgIe-YGBOyizE7V5Qx_xr-qb4ZQ0bijdK99XdBwtWThYTgIvXhvlq97yTLVesyJ15IVXnHwXs8xV4DpS-_A54bIi2v0kuAkqFT4S9L8GIl9fX4qhX3PVlJwHWI/s1600/1.JPG


Waziri wa Maliasili na Utalii Dr. Hamisi Kigwangalla amesema viongozi wote waliohusika na rushwa kwenye wizara hiyo watafikishwa kwenye mkono wa sheria.

Waziri ameyasema hayo alipotembelea hifadhi ya Serengeti katika pori tengefu la Loliondo ambapo amesema kuna kikundi ndani ya wizara kimekuwa kikiendesha vitendo vya rushwa kikihusisha wakurugenzi na mawaziri waliomtangulia.
“Ninafahamu kuwa kuna ugawaji wa vitalu kinyume na sheria ambao nimeusitisha na nitafuatilia vitalu alivyogawa waziri Nyalandu kinyume na sheria na mkurugenzi aliyekuwepo nitawachukulia hatua”, amesema Kigwangalla.

Kigwangalla amesema kuwa atafukua mafaili yote na kuwaondoa mmoja baada ya mwingine na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria wote waliohusika na vitendo hivyo ikiwemo kuwauza wanyama hai nje ya nchi.
“Siwezi kuendelea kufanya kazi mpaka nisafishwe hii nyumba kwasababu ni chafu nitaisafisha kwanza ndio niendelee na kazi aliyonipa mheshimiwa rais”, ameongeza.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post