Mjue Charlie Chaplin, Mwigizaji Mchekezaji wa zamani




Leo tunamuongelea mchekeshaji wa zamani ambaye aliacha historian duniani kwa kazi yake ya sanaa iliyowavutia watu wengi kipindi icho mpaka sasa

Charlie Chaplin ni miongoni mwa watu waliokuwa na vipaji hasa mpaka kuna baadhi ya watu wanasema hajatokea kama yeye mpaka sasa

Charlie Chaplin alizaliwa London, 16 Aprili 1889, wazazi wake waliofanya kazi katika sekta ya burudani alipokuwa na umri mdogo baba yake aliekuwa mlevi alipotea na baadaye mama yake alipata matatizona na akapelekwa kwenye hifadhi
Hii ilisababisha Charlie na nduguye kujilea wenyewe Mwaka 1910 Charlie alisafiri na kuelekea Amerika na kupata ujuzi katika sekta ya filamu kutokana na kipaji alichokuwa nacho alibuni alama mtindo wake wa uvaaji uliokuwa ukimtambulisha ni kofia ya bakuli, masharubu na nguo zinazofaa,


Charlie Chaplin akawa nyota kubwa na umaarufu wake ulienea duniani kote Charlie Chaplin alikuwa na uwezo mkubwa alitumia fedha, kuandika na kuelekeza filamu zake mwenyewe baadhi ya filamu zake maarufu zaidi ni pamoja na lights city ya Mwaka (1931) greater dictator ya Mwaka (1940)
Kutokana na uchekeshaji wake kuna watu wakiona picha yake tu wanacheka

Filamu yake ya Greater dictator ilikuwa inaongelea juu ya udikteta wa kikatili wa Hitler na Mussolini. Chaplin mwenyewe alicheza majukumu mawili alicheza kama myahudi aliyechaguliwa Pia alicheza kama "Adenoid Hynkel - dikteta wa Tomania ufahamu wazi wa Adolf Hitler Filamu hiyo ilifanyika mwaka mmoja kabla ya Marekani kuingia katika vita dhidi ya Ujerumani Hatimaye mamlaka ya Marekani waliamua kumruhusu kutumia visa yake ya kuingia Marekani baada ya kuzuiliwa kwa mda kwa sababu za kuukuunga mkono ukomunisti

Charlie Chaplin baadaye alisema hakuwa Mkomunisti lakini alikataa kuhukumu Wakomunisti kwa sababu hakupenda asili ya zama za McCarthy

Chaplin alikuwa na vipaji vya ajabu hii ilikuwa ni talanta iliyopatikana kupitia filamu zake za kimya Charlie Chaplin pia kutokana na kazi zake nzuri alipewa tuzo mwaka 1972 kwa alama yake ya muziki katika filamu ya 1952 Limelight Pia alipewa tuzo ya heshima mwaka 1972 ambayo picha ya mwendo aina ya sanaa ya karne hio
Charlie Chaplin alikuwa na watoto 11 kwa wanawake watatu tofauti na alikuwa na wanawake wengine kwa kibongo tunaita (michepuko) alikufa katika usingizi huko Vevey Uswisi siku ya Krismasi 1977 

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post