Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi ametia saini kandarasi mpya huku wale wanaomtaka kumnunua wakilazimika kugharamia thamani yake ya Yuro milioni 700.
Mchezaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 30 sasa atasalia Barcelona hadi msimu wa mwaka 2020-21.
Tangu alipojiunga na Barcelona akiwa na umri wa miaka 13, Messi ameisaidia Barcelona kushinda mataji manane ya ligi ya Uhispania na kushinda kombe la vilabu bingwa mara nne.
Messi ambaye kandarasi yake ya awali ilitarajiwa kukamilika mwaka ujao amefunga mabao 523 katika mechi 602 alichocheza.
Hivi majuzi alitunukiwa tuzo ya mchezaji aliyefunga mabao mengi baada ya kufunga mabao 37 katika ligi ya Uhispania msimu uliopita.
Tags
Michezo