Serikali Kununua Kondom Milioni 500 na Kusambazwa Nchini Bure

Serikali Kununua Kondom Milioni 500 na Kusambazwa Nchini Bure





Serikali inatarajia kununua kondomu milioni 500 zitakazosambazwa nchi nzima bure kwa lengo la kupunguza maambukizi ya Ukimwi ifikapo mwaka 2030.


Kondomu hizo zitasambazwa bila malipo ambapo kutakuwa na mashine maalumu zitakazofungwa kwenye maeneo ya baa, nyumba za kulala wageni, migodini na katika kumbi za burudani.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa mkakati wa kitaifa wa kondomu, Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Neema Rusibamaila, amesema kondomu hizo zitanunuliwa kupitia fedha za Global Fund.

“Takwimu za mwaka 2011/12 zinaonyesha asilimia 69 ya wanawake na asilimia 77 ya wanaume wanafahamu kwamba kondomu inaweza kuzuia VVU lakini ni asilimia 27 tu ya watu wenye wenza zaidi ya mmoja walitumia kondomu walipofanya ngono mara ya mwisho,” amesema. 

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post