Muigizaji na mchekeshaji Bongo, Idris Sultan ameandika barua ya wazi kwenda kwa aliyekuwa muigizaji wa filamu nchini Steven Kanumba.
Katika barua hiyo, Idris ameonyesha kuwa amewahi kuwa shabiki mkubwa wa marehemu na alihudhuria mazishi yake miaka kadhaa iliyopita. Kabla ya kuandika ujumbe huo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, muigizaji huyo aliyepata dili la kuigiza filamu Hollywood alianza kwa kupost video akiwa na muigizaji Elizabeth Michael aliyehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela.
Dear Kanumba,
Najua ulikua hunijui ila nilitembea kwa miguu kutoka mbezi kimara mpaka kinondoni kuja kukuzika. Ni mda mrefu sana umekua ukitembea na sisi kuomba upumzishwe, sasa naamini utapumzika kabisa. Allah akufanyie wepesi na milele utabaki mioyoni mwetu. Tulifunga njia, kazi na hata kuhema vizuri wengine tulishindwa na tukapata depression kubwa sanaaaa yote kwasababu ulitugusa katika mfano usioelezeka. Naamini haki yako sasa imepatikana na namuombea sana mama yako apewe nguvu na amani ya moyo. Finally Rested.
Ni mimi wako katika matumaini ya urithi wa ufalme wa movie Tanzania, Idris Sultan
Tags
Muziki